SPLA : Portail de la diversité culturelle
Cultures-Vanuatu

Kale ya Washairi wa Pemba

Kamange na Sarahani =
Abdilatif Abdalat (Editor)
  • Kale ya Washairi wa Pemba

Date de sortie : Dimanche 01 janvier 2012
Genre : Recueil de poésie

ISBN du livre : 9789987080854
Pages : 150
Pays principal concerné : Rubrique : Littérature / édition

Kale ya Pemba ni kale ya Waswahili na mazingira yao. Maandiko machache ya Abdulrahman Saggaf Alawy na AliAbdala El Maawy yameonesha mazingira ya watu wa kale na mawazo yao. Kale hiyo si kale ya kabla ya Fumo Liyongo, bali ni kale ya akina Kamange na Sarahani. Kamange na Sarahani waliingia katika karne ya kumi na tisa na kufariki katika karne ya ishirini. Mashairi yao yalivuma pwani yote ya Afrika Mashariki. Mwandishi Abdulrahman Saggaf Alawy amefanikiwa kukusanya baadhi tu ya maandiko ambayo yote yameandikwa katika mtindo wa kale wenye kujali bahari ya vina, mizani na kibwagizo cha wazo moja. Kamange alipenda sana kutunga mashairi ya kujitoma, ya ushaha, ya utendaji na ukali wa mapenzi ya wanawake. Sarahani alipenda elimu na kusomesha, kuingia katika falsafa na kutoa mawaidha. Kale ya Washairi wa Pemba ni mkusanyiko mkubwa wa utajiri wa mashairi yenye kuchanganya lahaja mbalimbali za Kipemba, Kimvita, Kiamu, Kimrima, Kivumba na yametumia pia maneno yenye asili ya Kiarabu yatumikayo katika Kiswahili. Kale ya Washairi wa Pemba kimehaririwa na Abdilatif Abdalla kutoka Mombasa, mshairi wa Sauti ya Dhiki na mwenye kupendwa sana nchini Tanzania alikoishi miaka mingi akifanya kazi katika Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Mashairi ya washairi hawa ni changamoto kubwa kwa wasomi wa Kiswahili wa ushairi kwa upeo wa juu sana wa sanaa na umahiri wa lugha.
The Past of Pemba Poets. Kamange and Sarahani is a treasure of Swahili poetry from the two great protagonist Swahili poets, deeply immersed in Swahili dialects and literary and poetic culture.
Preserved since the 1964 Zanzibar revolution, they are collected here for the first time.

[Consulter la fiche de l'ouvrage sur le site Web de l'African Books Collective]

Partenaires

  • Alliance Française VANUATU
  • PACIFIC ARTS ALLIANCE
  • FURTHER ARTS

Avec le soutien de